Loading...

UCHAGUZI NIGERIA: BILIONEA ANAYETISHIA NAFASI YA RAIS BUHARI

Loading...
Kuna wagombea zaidi ya 70 ambao wanataka kumng'oa madarakani rais Muhammadu Buhari, lakini ni Atiku Abubakar pekee ambaye anaonekana mwenye ubavu.

Abubakar ni mtu maarufu nchini Nigeria kwenye nyanja za kisiasa na biashara.

Amefikia moja ya cheo kikubwa kabisa cha utumishi, makamu wa raisi, na pia ni tajiri mkubwa aliyenufaika na sekta ya mafuta.

Ofisi kubwa zaidi ya nchi hiyo, urais, umekuwa ukimpiga chenga. Ameshajaribu mara tatu kabla na kuangukia pua.

Jumamosi Februari 16, kwa mara nyengine tena, mwanasiasa huyo mwenye miaka 72 anatupa karata yake, akiwaahidi wananchi kuwa uzoefu wake katika siasa na biashara ni dawa ya changamoto za nchi.

Hata hivyo wakosoaji wake wanamhusisha na kashfa za matumizi mabaya ya fedha, na kudai hilo tu linatosha kumfanya asipewe hatamu katika nchi ambayo rushwa ni tatizo kubwa.

Amekanusha vikali tuhuma hizo akidai zina mkono wa siasa ndani yake.

Endapo atachaguliwa, changamoto kuu mbele yake zitakuwa ongezeko kubwa la ukosefu wa ajira, umasikini wa kutupwa, bunge lililotawaliwa na matabaka ya kikanda, na uchumi unaoyumba kutokana na kutegemea pakubwa sekta ya mafuta.

Amekuwa akipiga kampeni ya kujitofautisha na rais wa sasa, Buhari, ambaye amekuwa akilalamikiwa kwa shida za kiuchumi.

Wanaompinga Buhari wanadai kuwa katiba yake ya kubana matumizi, kutokubali mabadiliko kumekuwa ni kikwazo katika kuingoza na kuleta mabadiliko nchini Nigeria.

Wanasema kwa upande wapili, Abubakar, ni mtu rafiki na anayeshaurika na ana uwezo wa kuunganisha ulimwengu wa siasa na biashara, hali ambayo wafuasi wake wanadai inaweza kunyanyua uchumi na kuliunganisha taifa.
Na Edson Kingu.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UCHAGUZI NIGERIA: BILIONEA ANAYETISHIA NAFASI YA RAIS BUHARI UCHAGUZI NIGERIA: BILIONEA ANAYETISHIA NAFASI YA RAIS BUHARI Reviewed by By News Reporter on 2/15/2019 06:43:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.