Loading...
Jeshi la Polisi Mbarali limesema limemkamata mganga wa jadi anayedaiwa kuhusika na mauaji ya Rose Nguku(6) anayedaiwa kuuzwa na baba yake na baadaye kuuawa na kunyofolewa viungo vyake
Kukamatwa kwa mganga huyo kunafanya idadi ya watu walio mbaroni kwa tuhuma za mauaji hayo kufikia wanne
Wengine waliokamatwa ni Japhet Nguku, ambaye ni baba anayedaiwa kumuuza binti yake kwa Tsh. milioni 5, Andrew Mwambuluma, mfanyabiashara anayedaiwa kumnunua mtoto huyo na ndugu wa mfanyabiashara huyo anayemiliki shule ya sekondari iliyoko Mbalizi
Kamanda wa Polisi wa Mbeya, Ulrich Matei alisema chanzo cha mauaji hayo ni tamaa ya kutaka utajiri haramu
Kamanda Matei alisema bado wanaendelea na uchunguzi zaidi, ikiwamo kutafuta kiganja cha mkono wa marehemu, hivyo wamezuia mazishi hadi watakapokipata kiungo hicho.

Na Fatma Pembe.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
POLISI YAMTIA MBARONI MGANGA ALIYEHUSIKA NA MAUAJI YA MTOTO ALIYEUZWA BABA YAKE
Reviewed by By News Reporter
on
5/15/2019 07:07:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: