Loading...

RAIS TRUMP ATOA MWALIKO WA 'IFTAR' WHITE HOUSE YA MAREKANI

Loading...
Rais wa Marekani Donald Trump atoa mualiko wa "Iftar" mlo wa jioni kwa  waislamu waliopo katika ibada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ikulu White House

Wanadiplomasia kutoka katika mataifa tofauti ya kiislamu wanaowakilisha mataifa yao nchini Marekani waliarifiwa katika mlo huo ulioandaliwa kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika hotuba yake fupi rais Trump amekumbusha kuwa  mwezi wa Ramadhani unakumbusha  thamani  ya ushirikiano na umoja kwa waislamu wote ulimwenguni.

Tangu katika utawala wa rais Bill Cliton, George Bush na Barack Obama "Iftar" ilikuwa ikiandaliwa ikulu hadi mwaka 2016.

Ikumbukwe kuwa Rais Trump katika  miezi yake ya kwanza akiwa madarakani alipiga marufuku ya viza kwa raia kutoka katika mataifa kadhaa ya kiislamu.
Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIS TRUMP ATOA MWALIKO WA 'IFTAR' WHITE HOUSE YA MAREKANI RAIS TRUMP ATOA MWALIKO WA 'IFTAR' WHITE HOUSE YA MAREKANI Reviewed by By News Reporter on 5/15/2019 07:24:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.