Loading...

MFALME MSWATI WA SWAZILAND AOA MKE WA 14

Mfalme Mswati wa III na Mkewe Mpya, Siphelele Mashwama
Mfalme Mswati wa III wa Swaziland amemuoa binti wa wa waziri Jabulile Mashwama kama mke wa kumi na nne (14) wa Mfalme huyo ambaye anaitwa Siphelele Mashwama mwenye umri wa miaka 19.

Bibi harusi wa mfalme wa Swazi amethibitishwa na mwangalizi na muandaaji wa sherehe ya mfalme huyo, Hlangabeza Mdluli.

Aliweka waza kwamba bibi mpya wa mfalme yupo sasa huko New York Marekani, ambapo mfalme huyo mwenye miaka 49 anahudhuria Mkutano Mkuu wa Um
Loading...
ja wa Mataifa (UN).

Mdluli aliwaambia waandishi wa habari siku ya jumapili, wakati mfalme alikuwa akijaribu kusafiri na ndege kuelekea New York, kwamba mfalme amechagua rasmi mke mpya.

Siphelele ni Mke wa sasahivi wa mfalme Mswati na ni mdogo kiumri kuliko wake zake wote.

Wake wengine wa Mfalme Mswati hawa hapa katika orodha:-

  • Zena Mahlangu
  • Inkhosikati LaDube
  • Inkhosikati LaNtentesa
  • Inkhosikati LaMagongo
  • Inkhosikati LaMasango
  • Inkhosikati LaGija
  • Inkhosikati LaMbikiza
  • Nomonde Fihla
  • Inkhosikati LaMatsebula
  • Inkhosikati LaMotsa
  • Inkhosikati LaNganganza
  • Colile Nosiphe Magagula
  • Siphele Mwashama - Mke Mpya
MFALME MSWATI WA SWAZILAND AOA MKE WA 14 MFALME MSWATI WA SWAZILAND AOA MKE WA 14 Reviewed by By News Reporter on 1/30/2018 07:15:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.