Loading...
Kushoto Diego Maradona na Kulia ni Rais Trump wa Marekani. |
Mwanasoka nguli kutoka nchini Argentina, Diego Maradona amezuiliwa kuingia Marekani baada ya kumtukana Rais Donald Trump kwenye Kwenye kituo cha Televisheni ya Amerika ya Kusini.
Mwanasheria wake, Matias Morla alithibitisha hili katika kipindi cha habari za kitaifa kiitwacho 'Buenos Dias America' cha nchini humo.
Alisema Maradona alikataliwa kupewa Visa ya Marekani baada ya kufanyiwa mahojiano na kituo cha televisheni cha Venezuela 'TeleSur', ambako alizungumza mawazo yake juu ya rais wa Marekani.
Matias alisema: "Unaweza kufikiria, nilikuwa katika ubalozi na nikasema 'Diego, tafadhali usizungumze kuhusu Marekani," Bw. Morla alisema.
"Kwa sababu mahojiano yalikuwa na TeleSur na najua jinsi mambo haya yanavyoenda."
"Na swali la pili ni 'Unafikiri nini kuhusu Donald Trump'?"
"Alisema Donald Trump ni chirolita (neno la slang lenye maana ya tupu au mbumbumbu au mpumbavu)?'"
Morla alisema kuwa kufuatia maoni ya kushtua ya Maradona, alimwambia mchezaji huyo wa zamani, "Baada ya mahojiano haya mimi ndio nitakuwa muwakilishi wako huko Miami badala yako."
Wakati wa mahojiano, Maradona (57), alikuwa katika mchakato wa kuomba visa kwa Mataifa, ambayo hatimaye walimkatalia.
Mwanasoka huyo nguli kwa sasa anasimamia Al Fujairah, klabu inayomilikiwa na Falme za Kiarabu alihitajika kusafiri Miami, Florida, ili kukabiliana na kesi inahusisha mke wake wa zamani Claudia Villafane.
MWANASOKA MKONGWE MARADONA AZUILIWA KUINGIA MAREKANI KWA KUMTUKANA RAIS TRUMP
Reviewed by By News Reporter
on
2/04/2018 07:27:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: