Loading...

SHILOLE: NIKIFA SITAKI MWILI WANGU UFANYIWE MBWEMBWE

Loading...
Mwanamke wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka kupitia mtandao wake wa Instagram na kutoa sharti siku akifa kuwa hatataka mwili wake ufanyiwe mbwembwe Leaders Club.

Shilole amesisitiza kuwa hatataka mwili wake ufanyiwe mbwe mbwe Leaders Club badala yake anataka mambo yote yaishie msikitini kwa kuwa yeye ni mtoto wa kiislamu.

Wiki mbili zilizopita Mrembo Agnes Masogange alifariki dunia kwa kile kinachodaiwa kuwa ni Pumu na baada ya hapo mwili wake uliagwa Kwenye viwanja vya Leaders Club.

Kwenye mahojiano na Risasi Jumamosi, Shilole amesema yeye anatoa agizo kuwa, ikiwa ametokea amefariki dunia leo au kesho, kama siyo kuagwa nyumbani kwake Gongo la Mboto, basi aagwe msikitini.

"Mimi sitapenda kabisa taratibu za mazishi yangu zifanyike katika Viwanja vya Leaders, ni bora kama nyumba yangu itakuwa haijamalizika basi watu wakafanyie taratibu hizo msikitini kwa sababu mimi ni mtoto wa kiislam, siwezi kuagwa kwenye viwanja ambavyo watu wanakunywa na kuuza pombe".

Na Catherine Kisese.



Tuma neno 'HABARI' kwenda +255765112259 kupata habari za mastaa punde zinapojiri.
SHILOLE: NIKIFA SITAKI MWILI WANGU UFANYIWE MBWEMBWE SHILOLE: NIKIFA SITAKI MWILI WANGU UFANYIWE MBWEMBWE Reviewed by By News Reporter on 4/30/2018 09:57:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.