Loading...
Waziri mkuu wa Ubelgiji, Charles Michel, ameziomba msamaha nchi za Burundi, DR Congo na Rwanda kwa kuhusika na maelfu ya visa vya utekaji nyara wa watoto waliozaliwa na walowezi wa nchi hiyo zama za ukoloni.
Watoto hao wanaosadikiwa kuwa karibu 20,000 walichukuliwa kwa nguvu kutoka kwa mama zao waafrika na kupelelewa na kanisa katoliki na taasisi zingine zanchini Ubelgiji.
Baadhi ya watoto hao ambao walizaliwa miaka ya 1940 na 1950, hawakuwahi kupewa uraia wa Ubelgiji hali iliowafanya kuishi kama watumwa.
Akilihutubia bunge la nchi hiyo,Bw. Michel alikiri kuwa Ubelgiji ilikiuka haki ya kimsingi ya watoto hao, kwa kuwachukulia kama tisho kwa mfumo wa ukoloni.
Ubelgiji iliwavua uraia wao, kuwabagua na kuwatenganisha na jamaa zao.
"Hatua hii itatusaidia kutambua rasmi sehemu ya historia yetu ya kitaifa,"alisema katika taarifa yake.
Bunge limesema kuwa hatua yake ya kuomba msamaha watu wa asili ya kiafrika waliotekwa na kupelekwa nchini humo wakiwa watoto wadogo lazima isaidie kuimarisha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo.

Na Haika Gabriel.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KWANINI UBELGIJI IZIOMBE MSAMAHA KONGO, UGANDA NA RWANDA?
Reviewed by By News Reporter
on
4/05/2019 09:22:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: