Loading...

SAUDI ARABIA YAWANYONGA RAIA 37 KWA MAKOSA YA UGAIDI

Loading...
Saudi Arabia imesema kuwa imewanyonga raia wake 37 baada ya kuhukumiwa kwa ugaidi katika nchi hiyo ya Kifalme, ambayo ni mojawapo ya nchi zinazoongoza duniani katika kutekeleza adhabu ya kifo. 

Hukumu hizo za kunyongwa zilitekelezwa Riyadh, miji mitakatifu ya kiislamu ya Mecca na Medina, mkoa wa kati wa Qassim na Mkoa wa Mashariki. 

Taarifa iliyochapishwa na Shirika la Habari la Saudia imesema watu hao walinyongwa kwa kufuata nadharia za kigaidi na itikadi kali na kwa kuunda makundi ya kisiri ya kigaidi ili kuvuruga na kuudhoofisha usalama wa nchi. 

Imesema mtu mmoja alisubishwa baada ya kunyongwa, adhabu ambayo hutolewa hasa kwa makosa makubwa ya uhalifu. Hukumu za kifo katika nchi hiyo ya kihafidhina zaidi kawaida hutekelezwa kwa kukata kukata kichwa.
Na Tariq Mohamed.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SAUDI ARABIA YAWANYONGA RAIA 37 KWA MAKOSA YA UGAIDI SAUDI ARABIA YAWANYONGA RAIA 37 KWA MAKOSA YA UGAIDI Reviewed by By News Reporter on 4/24/2019 08:20:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.