Loading...

UNAUA IPHONE YAKO KWA MAKOSA HAYA YA KUCHAJI

Loading...
Simu aina ya Iphone
Kama vile watu wa zamani, iPhones za zamani zilikuwa zina wakati mgumu sana kutunza chaji zao - na sehemu ya sababu kubwa ni namna tunavyozichaji. Baadhi ya tabia zetu zinazoonekana kutokuwa na madhara ndio zinazochangua kuua kimya kimya betri za aina ya Lithium-ion zilizopo katika simu za iPhone.

Kuchaji mpaka asilimia 100%

Kama simu yako kupungua chaji yake chini ya 90%, unahitajika kutulia. Kudumisha simu kwa kuchaji mpaka ijae chaji sio ndio kigezo cha betri ya simu yako kuwa imara. Ukweli ni kwamba, wataalam wanashauri kuruhusu simu ipungue chaji kwa asilimia kati ya 30 hadi 80. Ndio ambapo simu yako itafanya kazi kwa ufanisi mzuri. Kwahiyo usiwe unailazimisha usiku kuijaza chaji mpaka 100% na bado unaendelea kuijaza tu.

Unaiacha simu yako ife

Betri aina za Lithiumu ioni zinaharibika kiurahisi zikiwa na chaji kiasi kidogo, hivyo unapaswa kuepeku kupata onyo la "Low Battery" mara kwa mara. Kila kuisha kwa chaji ya betri mpaka mwisho kunaua betri ya simu yako taratibu. Hivyo imeshauriwa, na Apple na wataalam wengine kwamba unaruhusiwa kuiacha isiwe na chaji betri la simu yako mara 2 kwa mwezzi ili kuendeleza ubora wake na sio mara kwa mara.

Unapasha joto betri yako kupita kiasi

Sawa, hii haihusiani na swala la kichaji simu. Lakini bado ni muhimu sana.
Pengine unaanza kuona simu yako inakwama kwama baada kuiweka juani. Hiyo ni kwasababu betri za iPhone zinachukia sana joto kali, na zitafanya kazi ya ziada zikiwa katika mazingira ya joto na baridi.
Kwa mujibu wa kampuni Apple, mazingira rafiki ya vifaa vya vinavyotengenezwa na kampuni hiyo ni kati ya jotoridi 32 hadi 95. Mbali na hapo simu yako itakuwa kama dubwashwa na haina kazi tena kwa kipindi fulani.

Unaendelea kuvisha kasha kipindi cha kuchaji

Wakati unachaji simu, kama simu unahisi ni ya moto sana, huende kasha la simu yako limeambukizwa joto na simu yako wakati wa kuchomeka chaji. Hivyo ipe simu yako nafasi kwa kuitoa kasha lake.

Unatumia chaja sio sahihi

Chaja ya simu za apple zimetengenezwa kukata umeme wakati betri ikiwa na asilimia 100%, lakini hizo zilizotengenezwa na makampuni mengine hazina uwezo huo na hata kusababisha madhara na kuua betri yako.

UNAUA IPHONE YAKO KWA MAKOSA HAYA YA KUCHAJI UNAUA IPHONE YAKO KWA MAKOSA HAYA YA KUCHAJI Reviewed by By News Reporter on 2/02/2018 12:24:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.