Loading...

WANASAYANSI WAUNDA BINADAMU ASIYEPATA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

Mwanasayansi kutoka Uchina ambaye amedai kuwa amesaidia kuzalisha watoto wa kwanza ambao chembe zao za jeni zilihaririwa kabla ya kuzaliwa na kwamba hawawezi kuambukizwa Ukimwi, ameshutumiwa vikali na madai yake kutiliwa shaka.

Prof He Jiankui anadai kwamba wasichana hao pacha, waliozaliwa wiki chache zilizopita, vinasaba vyao (DNA) vilifanyiwa ukarabati wakiwa bado ni viinitete kuwawezesha kutoambukizwa Virusi Vinavyosababisha Ukimwi (VVU).

Madai yao aliyoyatoa kwenye kanda ya video iliyosambazwa na shirika la habari la Associated Press hayajapigwa darubini na yamewaghadhabisha wanasayansi wengine.

Wamesema wazo hilo lenyewe ni la kuogofya.
Loading...
amily: "verdana" , sans-serif;">
Kazi kama hizo za kisayansi, za kuhariri jeni za binadamu, zimepigwa marufuku katika mataifa mengi.

Wanasayansi wanaamini kwamba uhariri wa jeni unaweza kuwaepushia watu magonjwa ya urithi yanayotokana na vinasaba, kwa kufuta chembe za jeni zinazosababisha magonjwa hayo au hata kuzifanyia ukarabati mtoto akiwa bado ni kiinitete.

Lakini wataalamu wana wasiwasi kwamba kuhaririwa huko kwa jeni kunaweza kusababisha madhara makubwa sio tu kwa mtoto mwenyewe bali pia vizazi vya baadaye ambavyo vitayarithi marekebisho yaliyofanywa na wanasayansi kwenye vinasaba.

Katika mataifa mengi, ikiwemo Uingereza, kuna sheria zinazoharamisha kuhaririwa kwa jeni hata katika mchakato wa kuwasaidia binadamu kutungisha mimba.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WANASAYANSI WAUNDA BINADAMU ASIYEPATA MAAMBUKIZI YA UKIMWI WANASAYANSI WAUNDA BINADAMU ASIYEPATA MAAMBUKIZI YA UKIMWI Reviewed by By News Reporter on 11/28/2018 06:37:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.