Loading...

UGONJWA WA KIMETA WAIBUKIA KENYA, WATU 2 WATHITISHWA KUFARIKI

Loading...
Watu 2 kutoka kaunti ya Meru wameripotiwa kufariki dunia kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa kimeta 

Idara ya afya kaunti hiyo pia ilithibitisha kuwa watu 9 wameambukizwa ugonjwa huo na wamelazwa katika hospitali ya Muthara Level Five. 

Waathiriwa wanasemekana kula nyama ya ng'ombe aliyefariki kutokana na maradhi yanayodhaniwa kuwa ya kimeta katika kijiji cha Muthara.

"Watu wawili wamefariki kutokana na kile kinachoaminika kuwa maradhi ya ugonjwa wa kimeta, sampuli zimechukuliwa ili zifanyiwe vipimo katika taasisi ya utafiti wa matibabu, KEMRI," Mkurugenzi mkuu wa mawasiliano Purity Nkirote alisema. 

Ingawa maafisa wa afya hawajabaini chanzo cha ugonjwa huo, imesemekana kuwa visa vya kuzuka kwa ugonjwa wa kimeta viliripotiwa kwa wingi wakati wa likizo ya pasaka.
Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UGONJWA WA KIMETA WAIBUKIA KENYA, WATU 2 WATHITISHWA KUFARIKI UGONJWA WA KIMETA WAIBUKIA KENYA, WATU 2 WATHITISHWA KUFARIKI Reviewed by By News Reporter on 4/26/2019 09:42:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.