Loading...

KATIKA HILI LAZIMA TUBADILIKE - Na Siri ya Utajiri

Loading...
Katika hili lazima tubadilike, mtu unakuta anaendelea na MATENDO yale yale, TABIA zile zile, MARAFIKI wale wale, MANENO yale yale na MAWAZO yale yale halafu anasubiri mabadiliko katika maisha yake.

Ni kweli kesho yako ni bora kuliko leo kwa maana ya kwamba kuna matumaini ya maisha bora kwa kesho. Lakini jambo hili halitokei kwa MIUJIZA, lazima uhusike kuitengeneza kesho yako. Fursa ipo inakusubiri tu wewe uchue hatua.

Mwenendo wako wa leo kimatendo, kifikra na mawazo lazima uwe TOFAUTI na wa jana. Maisha yako yatabadilika pale tu utakapokuwa TAYARI kubadilika. Kama maisha uliyonayo leo unatamani yabadilike basi tambua kuwa unalo JUKUMU la wewe kubadilika pia.

Kuendekeza tabia zile zile na matendo yale yale huku ukitarajia mabadiliko katika maisha yako ni kujidanganya. Chukua HATUA!

You Deserve The Best!
Vicent Stephen
KATIKA HILI LAZIMA TUBADILIKE - Na Siri ya Utajiri KATIKA HILI LAZIMA TUBADILIKE - Na Siri ya Utajiri Reviewed by By News Reporter on 2/07/2018 11:05:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.