Loading...

FAHAMU JINSI YA KUISHINDA TABIA MBAYA - Na Siri ya Utajiri

Loading...
Kuna watu wanatamani sana kubadili tabia fulani ambazo hawazipendi lakini kila jitihada hazizai matunda. Wanaazimia kuacha, siku ya kwanza wanajitahidi lakini siku ya pili wanarudi kule kule. Wanaumia kwa nini wanashindwa kila wanapojaribu.

Katika mazingira haya nini kifanyike? Tabia ni mazoea uliyojenga kwa muda mrefu ndani ya akili yako. Mazoea haya yana mizizi ya kisaikorojia ndani kwako. Tabia humtunuku mtendaji pale anapokuwa ameitikia wito. Malipo haya inaweza kuwa  kujisikia furaha au chochote kile unachokipata ama kuhisi baada ya kuwa umetenda. 
Inafika wakati mtu anazoea malipo (tuzo) haya kiasi kwamba anatamani kila wakati kuitenda tabia hiyo.

Watalaamu wa sayansi ya tabia wanasema, si jambo rahisi kubadili tabia ila pia ni jambo linalowezekana. Njia mojawapo inayopendekezwa ili uweze kubadili tabia fulani ni kutafuta kitu mbadala ambacho utakifanya na kikupe tuzo (malipo) ile ile kama unayoipata kutoka katika tabia unayopambana kuiacha.

Ukishindwa kufikia ile tuzo mfano furaha uliyokuwa unaipata basi ni rahisi sana kurudi katika ile tabia unayotaka kuibadili. Hakikisha jambo mbadala unalofanya likupe kiasi kile kile cha furaha (Malipo). 

You Deserve The Best!
Vicent Stephen
FAHAMU JINSI YA KUISHINDA TABIA MBAYA - Na Siri ya Utajiri FAHAMU JINSI YA KUISHINDA TABIA MBAYA - Na Siri ya Utajiri Reviewed by By News Reporter on 2/15/2018 01:05:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.